Moja ya Transifoma iliyopo katika Kituo cha Umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam (Ubungo Grid Sub Station) imeungua moto jioni hii (Jioni ya jana). Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Naibu Mkurugenzi wa Tanesco, Bi. Sophia Mgonja amesema kuwa, kutokana na hitilafu hiyo Jiji la Dar es Salaam na Visiwa vya Zanzibar vitakosa umeme kwa siku kadhaa. Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo, Mgonja alisema lilitokea baada ya kifaa cha kurekebisha nguvu ya umeme kiitwacho Reactor kuungua.Picha hizi zinawanyonyesha wafanyakazi wa kikosi cha zima moto wakizima moto katika Transifoma iliyokuwa ikiungua.Picha kwa hisani ya Kulwa Mwaibale/GPL.
No comments:
Post a Comment