Thursday, November 10, 2011

CHADEMA YAAHIRISHA MAANDAMANO YAKE LEO JIJINI DAR ES SALAAM:

Mwita mwikabe ambaya ni mkurugenzi wa taifa wa sera na utafiti wa Chadema akifafanua kwa waandishi wa habari sababu za kuahirisha maandamano ya leo.

Mwita mwikabe ambaya ni mkurugenzi wa taifa wa sera na utafiti wa Chadema akifafanua kwa waandishi wa habari sababu za kuahirisha maandamano ya leo.
Mwenyekiti wa BAVICHA Ndg.John Heche akizungumza na wanahabari juu ya maandamano na sababu za kusitisha maandamano hayo.
Wafuasi wa Chadema wakitawanyika kwa amani baada ya kuombwa na mwenyekiti taifa na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe kuwa waahirishe ili akamilishe mazungumzo na wakuu wa polisi.
Mmoja wa askari polisi akiwa kazini leo wakati Chadema walipoahirisha maandamano yao Kimara Dar es salaam leo.
Askari polisi akiwa kazini leo
 -
Maandamano makubwa yaliyoitishwa na Chadema leo yameahirishwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ombi la mwenyekiti wa chama hicho taifa aliyewataka wanachama na wapenzi wa chama chake waliokuwa tayari kwenye sehemu ya kuanzia maandamano kimara kuahirisha ili amalizie mazungumzo na maafisa wa jeshi la polisi waliomuomba asitishe maandamano hayo ili kutoa fursa ya maongezi, jambo ambalo Mheshimiwa Mbowe Amelifanya .

No comments:

Post a Comment