Monday, September 26, 2011

UTANI UNAPOMPATA MTANIAJI; RAGE VS MAGGID WA IRINGA:

MTANI WANGU ADEN ACHANA NA BASTOLA RUDI KWENYE JAMBIA:
Aden Rage akiwa na bastola yake kiunoni.

Mtani wangu Aden Rage, hivi tangu lini Mnyamwezi wa Urambo akabeba bastola kiunoni? Na unafanyaje bastola inapoishiwa risasi? Yaweza kuwa mauti yako.  Tuliopitia jeshini tunajua  kuwa kuna silaha zenye singe. Bastola haina singe.

Rage achana na bastola, rudi kwenye jambia, silaha yetu ya jadi. Na kwenye mapambano ya ana kwa ana na hususan mtu kwa mtu , jambia ndio silaha ya uhakika. Na pambano la kutumia jambia lina hatua mbili; mosi, kumshambulia adui kwa kutumia ubapa wa jambia. Pili, ikitokea pambano likawa gumu na hata adui akakamata jambia, basi, mara tu jambia likiwa mikononi mwa adui, unachotakiwa ni kuchomoa sime na kumwacha adui akiwa amebaki na mfuko wa sime.

Na mapambano mengi Afrika hayafikii mtu akachomoa sime! 
Sasa mtani wangu Aden,  iweje umeamua kuwatisha Wanyamwezi wenzako kwa bastola?

Any way, yamkini, Aden Rage lilikuwa jina maarufu sana pale klabuni kwetu Simba Sports Club,  Msimbazi, Kariakoo. Leo  umaarufu wa Mnyamwezi wa Urambo Aden Rage umeenea Unyamwezini na Usukumani kote,  na ukafika mpaka Manyema ya Kigoma. Kisa? Bastola kiunoni. Wanyamwezi bure kabisa!

Maggid, 
Iringa.

No comments:

Post a Comment