Sunday, September 25, 2011

DR.SHEIN AFUNGUA RASMI SHULE YA SEKONDARI YA WAMA NAKAYAMA ILIYOPO WILAYANI RUFIJI:

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mawaziri Dr.Ali Mohamed Shien akifungua rasmi shule ya sekondari ya Wama Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati wilayani Rufuji Mkoa wa Pwani. Kushoto ni mwenyekiti wa WAMA, mama Salma Kikwete akishuhudia ufunguzi huo.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dr.Ali Mohamed Shein (katikati), akipatiwa maelezo ya shule hiyo na mwalimu mkuu, Twaha Twaha (Kulia). Kushoto ni mwenyekiti wa WAMA, mama Salma Kikwete.
Mwenyekiti wa WAMA, mama Salma Kikwete, akiwa na baadhi ya waasisi wa UWT.
Mkuu mpya wa mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza, akiwakaribisha wageni ukumbini.
 
Katibu wa WAMA, Daud Nasib, akiongea katika hafla ya ufunguzi wa shule hiyo.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Wama Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati wilayani Rufiji mkoa wa Pwani akimwonesha mgeni rasmi moja ya mazoezi wanayojifunza shuleni hapo kuhusu matumizi ya Computer.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mawaziri, Dr. Ali Mohamed Shein, akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa mwenyekiti wa WAMA, mama Salama Kikwete.
Mwenyekiti wa WAMA, mama Salma Kikwete, akiwaaga wanafunzi baada ya ufunguzi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment