Friday, August 12, 2011

SUGU ALIPUA BOMU BUNGENI;NI KUHUSU STUDIO ALIYOITOA RAIS KIKWETE KWA WASANII WATANZANIA:

Mr.II a.k.a Sugu.
Mbunge wa mbeya mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu kama Sugu, amesema jina la Rais Kikwete litachafuliwa na kuonekana kuwa anafanyakazi chini ya maslahi ya watu binafsi badala ya umma kama studio aliyoahidi kiongozi huyo mkuu wa nchi kwa ajili ya kusaidia wasanii itabaki kuwa mikononi mwa taasisi binafsi ya nyumba ya vipaji THT.
Aidha Sugu alihoji uhalali wa nyumba iliyotolewa na serikali kwa ajili ya studio hiyo kugeuzwa kuwa makao makuu ya THT wakati akiwasilisha bungeni bajeti ya kambi ya upinzani ya wizara ya habari, utamaduni, vijana na michezo kwa mwaka 2011/2012 mjini Dodoma.  
Habari zaidi Soma VIJIMAMBO:

No comments:

Post a Comment