Ulishwahi kusikia kauli kama hii; "Nakwenda mjini"..?? Hiyo ni kauli ya mkaazi wa jiji la Dar es salaam akiaga kutoka, aidha, Tandika, Kigogo, Mbezi, Magomeni, Gongo la mboto, Mbagala ama sehemu nyingine yoyote ile ya Dar kwa lengo la kwenda maeneo ya kati kati ya jiji hilo, kama vile Kariakoo au Posta. Mjini kwenyewe ndiyo kama hivyo panavyonekana pichani. Shimo hili lipo katika makutano ya barabara ya Bibi Titi Mohammed na barabara ya Kisutu (Mbele ya jengo linaloitwa Elia Complex). Maji hayo si ya mvua bali ni maji machafu yanayotiririka toka kwenye chemba za maji taka hasa kuanzia maeneo ya karibu na Haidary Plaza. Mjini kwetu bana, daah.., Kila kitu Nyerere...!
No comments:
Post a Comment