Thursday, August 11, 2011

ALMANUSURA GARI HILI LITEKETEE KWA MOTO:

Kama gari hili lisingekuwa na kifaa cha kuzimia moto 'Fire Extinguisher' hakika lingeteketea kabisa, watch out drivers and vehicles owners.
Wasamalia wema wakiwemo askari wa kampuni ya ulinzi na usalama ya Ultimate Security wakisaidia kuzima moto uliowaka katika gari hiyo pichani usiku wa jana maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa watu waliokuwepo katika tukio hilo, chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyotokea kwenye betri ya gari hiyo, hata hivyo, hakuna majeruhi, hakuna aliyepoteza maisha.

No comments:

Post a Comment