Wednesday, July 6, 2011

VUMILIA KUPAMBANA NA TSHALLA MUANA KATIKA TUNZO ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:

 Mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya nchini Bongo, Vumilia Abraham Mwaipopo a.k.a Vumi a.k.a Queen of the Night anatarajia kupambana na nguli wa muziki wa Mutuashi barani Afrika, Elizabeth Modiakai 'Tshalla Muana' katika tunzo za Afrika mashariki na kati zinazotarajiwa kufanyika August 20 mwaka huu jijini Nairobi - Kenya.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tunzo hizo, Kampuni ya Golden Dreams ya Nairobi - Kenya ilimtaja Vumi katika tunzo ya mwanamziki bora wa muziki wa Rhumba akichuana na Tshalla Muana pamoja na Masha Mapenzi wa Kenya.
Vumi (Tanzania) ameingia katika mchakato huo kutokana na wimbo wake wa tatizo umasikini, Tshalla Muana (Congo) ameingia na wimbo wa Malozi wakati Masha (Kenya) akiwa ameingia na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Kala Ulele.                                                                                  











                                                               Vumi.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment