Monday, July 25, 2011

TUNZO MBALIMBALI ZATOLEWA KATIKA BIRTHDAY PARTY YA MACHOZI BAND YA KUTIMIZA MIAKA 6:



Ijumaa ya tarehe 22 July katika bustani ya Nyumbani Longue, Machozi band ilisherehekea Annivesary ya miaka 6 tangu kuanzishwa kwake.

Sherehe hiyo pia iliambatana na utoaji wa tunzo mbalimbali kwa wanamziki na wafanyakazi wa Machozi Band ambapo tunzo hizo ziligawanyika katika vipengele vifuatavyo:
Muimbaji Bora,
Mfanyakazi Bora,

Mwanamuziki mwenye nidhamu,

Mwanamuziki aliedumu kwa muda mrefu na Band,

Mwanamuziki mwenye Talent zaidi.


Mwinyigoha akikabidhiwa tunzo ya mwanamuziki anayejipenda na mwenye mwonekano safi kwa kipindi chote ambacho yupo kazini.

Shamim akimkabidhi Mbwana Mponda tunzo ya mwanamziki aliyedumu na bendi kwa muda mrefu zaidi kuliko wengine. Mponda anapiga Bass Guitar tangu bendi hiyo ilipoanza mpaka sasa.

Jonico Flower, akipokea tunzo ya Best Vocalist.
Tunzo ya mfanyakazi bora ilikwenda kwa jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la 'dudu'. Tunzo hiyo ilipokelewa na mkewe kwa niaba ya mumewe ambaye alikuwa anaendelea na mzigo hapo hapo wakati tunzo hizo zikitolewa.

Huyu ndiye mwenye tunzo hiyo, Mr Dudu, akisherehekea na mkwewe.

Mwanamziki mwenye nidhamu zaidi, jamaa anaitwa Jules.

Raia wengine waliohudhuria.

No comments:

Post a Comment