Sunday, July 3, 2011

SIMBA YANG'ANG'ANIWA KOO NA RED SEA YA ERITREA:

 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza leo katika uwanja wa Taifa kushuhudia kabumbu kati ya wekundu wa msimbazi (Simba Sports Club) ya hapa Bongo na Red Sea ya Eritrea katika mashindano ya Kagame Castle Cup ambapo mnyama Simba alishindwa kufurukuta kwa wageni wake hao wa Eritrea baada ya kutoka sare ya bila kufungana a.k.a tasa (0 - 0).

 Beki maridadi wa Red Sea ya Eritrea, Flimon Tsegay (Katikati) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Simba, Rajab Isihaka (Kulia) huku golikipa wa timu hiyo ya Red Sea, Daniel Goitom akiwa makini kuangalia yasije yakatokea mengine.
 Ulimboka Mwakingwe, Mshambuliaji wa Simba (Kulia), akijaribu kumtoka beki wa Red Sea, Flimon Tsegay.

Mussa Hassani Mgosi akiwa na mpira.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment