Thursday, July 28, 2011

SERGIO AGUERO AWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI NDANI YA JIJI LA MANCHESTER:


Sergio Aguero.
Sergio Aguero amemalizana na matajiri wa Manchester City hivyo kutangazwa kuwa mchezaji rasmi wa kikosi cha Roberto Mancini.
City wamekubali kulipa £38 million kwa Atletico Madrid kwa ajili mkwe wa Diego Maradona, ambaye amesaini mkataba wa miaka 5 huku akiwa anapata mshahara wa £200,000 kwa wiki, hivyo kufanya thamani ya jumla ya uhamisho wake kuwa zaidi ya £85million.
Uhamisho huu wenye thamani £85m wa Aguero, 23, ambaye atavaa jezi no.16 ndio wa ghali zaidi katika historia ya vilabu vya jiji la Manchester.

Alipotua katika jiji la Manchester.
Muargentina huyo alisafiri kutoka kwao siku ya Jumanne usiku mara baada ya klabu mbili kumalizana, na alitumia mtandao wa Twitter kuelezea kuwasili kwake ndaji ya jiji la Manchester.
Aliandika; “Nimefika jijini Manchester kukamilisha details za ofa ya City. Kila kitu kipo sawa, muda mchache ujao nitawaambia zaidi.”

2 comments:

  1. Nipo upande wa pili wa jiji la manchester---OLD TRAFFORD-The theatre of dreamz.....ila huyu dogo namkubali!!!

    ReplyDelete