Friday, July 29, 2011

MKALI LUDACRIS 'ALIPODONDOKA' BONGO JANA JIONI:

Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip Hop,ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Bryian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili jana jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwl Jk Nyerere na kupokelewa na Wenyeji wake. Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Fiesta 2011,Serengeti Primeum Lager.
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group, Balozi Kidamba, akisalimiana na kumkaribisha mwanamuziki Ludacris, kwenye hoteli ya Kempinsk mara tu baada ya kuwasili jioni ya jana akitokea nchini Marekani.
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group, Balozi Kidamba, akimuongoza mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk jioni ya jana mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onyesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar manamo July 30.
Mwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group, Balozi Kidamba, akiwafafanulia jambo Wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya jana akitokea nchini Marekani.
Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Wana Wa Clouds TV jioni ya leo.
Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni ya jana ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.

No comments:

Post a Comment