Thursday, June 16, 2011

UTABIRI WANGU: AZAM FC YA DAR ES SALAAM-TANZANIA NI MOJA YA TIMU AMBAZO ZITAZOKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA MIAKA MICHACHE IJAYO:

Umakini (seriousness), kujiamini (confidence), kujidhatiti (Commitment) na mikakati ya mipango enedelevu juu malengo waliyojiwekea ni silaha kubwa ya kusonga mbele kimaendeleo ya timu hii inayocheza ligi kuu ya Tanzania, AZAM FC. Moja ya vitu vya msingi ambavyo mara kwa mara Azam FC imekuwa ikiwapatia wachezaji wake ni pamoja na kwenda Gym kwa ajili ya mazoezi ya viungo. Fuatilia hapo chini:

Kocha wa magolikipa wa Azam FC, Idd Abubakary akiwaelekeza magolikipa wa timu hiyo (Daudi Mwaisongwe na Mwadini Ali Mwadini ambaye pia ni golikipa wa timu ya Taifa ya Zanzibar) wakati wa mazoezi ya gym katika gym ya Fitness Centre ya kinondoni jijini Dar es salaam. Timu hiyo imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania inayotarajiwa kuanza mwezi August mwaka huu.


Mchezaji wa Azam FC kutoka Ivory Coast, Kipre Helman Cheche akifanya mazoezi katika gym hiyo.

Kocha mkuu wa timu ya Azam FC, Stewart John Hall, akimwelekeza mchezaji wa timu yake, Malika Ndeude jinsi ya kufanya mazoezi katika mashine.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment