Tuesday, June 21, 2011

OLD SCHOOL;FLASHBACK;OLD IS GOLD;YA KALE NI DHAHABU NDANI YA MWANZA:

Nyumba ya enzi za mwalimu jijini Mwanza.

Nyumba hii ya 'enzi za mwalimu', a.k.a nyumba ya siku nyingi a.k.a nyumba ya kale a.k.a Old is Gold a.k.a Flashback a.k.a Old School inapatikana katika eneo moja linalojulikana kwa jina la Makoroboi jijini Mwanza.

 Sababu iliyopelekea kuwepo hapa kama 'New post' katika blog hii ni ustadi, umakini, werevu na mpango madhubuti wa wajenzi wa nyumba hii ya kale iliyoweza kudumu mpaka leo bila ya kuteteleka wala kuweka nyufa.Kama inavyoonekana pichani, nyumba imejengwa juu ya mawe na ni umbali wa kama mita 150 kutoka usawa wa ardhi kwenda juu ilipo nyumba hiyo lakini cha ajabu zaidi, iwe jua kali sana, upepo mkali sana, ama hata mvua kali sana yenye muungurumo mzito na miale mikali ya mwanga wa radi nyumba hiyo bado iko ngangari. Je, hivi wajenzi wa namna hii wamekwisha kabisa nchini mwetu? Au nyumba hii haikujengwa na watanzania? Iweje sasa majumba na maghorofa siku hizi yanaporomoka tu bila ya sababu za msingi? Mwenye data za kutosha kuhusuana na hili achangie mada hii kwa njia zifuatazo:

1. Kwa kutuma maoni (Post a Comment)
3. Simu no; (+255)712 165500, (+255)767 165501

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

2 comments:

  1. hizo nyumba ndio utamaduni wetu sie kwni ni utambulisho wa mwanza.

    ReplyDelete