Vodacom Miss Dar City Centre 2011, Alexia William akipunga mkono mara baada ya kutawazwa kuwa mlimbwende mpya wa kanda hiyo. Wengine, wa kwanza kushoto ni mshindi wa pili, Salha Israel na wa kwanza kulia ni mshindi wa tatu, Jenifer Kalokola. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala, ndugu Jerry Slaa akimkabidhi mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Centre Alexia William zawadi ya shilingi Milioni 1/- za kitanzania zilizotolewa na waandaaji wa shindano hilo. Pembeni ni mke wa meya Slaa. Mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Centre, Alexia William akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa pili, Salha Israel (Kushoto) na mshindi wa tatu Jenifer Kalokola.
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click Post comments.
No comments:
Post a Comment