Monday, September 10, 2012

PICHA ZAIDI KATIKA "ALLY REHMTULLAH 2013 COLLECTION (AR2013):




Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha Vito vyenye Madini ya Tanzanite yanayochimbwa nchini Tanzania wakati wa raundi ya kwanza ya onesho la 'Ally Rehmtullah 2013 Collection.(The Tanzanite Experience).
 
Pichani Juu na Chini ni Models wa kiume wakionesha Mavazi ya Street Souls ambao ni mmoja wa wadhamini wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'.
    
Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'. 


Mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Ally Rehmtullah, akijitambulisha baada ya Model kuonesha Collection yake mpya ya Mwaka 2013 katika Onyesho la aina yake katika hoteli ya Serena jijini Dar.
 
 Warembo waliokuwa wakikaribisha Wageni kutoka kampuni ya DULUX. Mmmh, hii kiboko, baaab kubwa.
 
 Mboni Masimba wa 'The Mboni Talk Show' ya EATV, a.k.a Kim Kardashian wa Bongo na rafiki.
 
 Evelyn na Eskado Bird. Halla at you guys.
 
Dadaz...!! Bhhaaass...!!
 
Sweet Legs.

MC Taji Liundi akitoa utambulisho wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection' iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya wadau kutoka ndani na nje ya nchi.

Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors ambao ni Wadhamini wakuu wa 'Ally Rehmtullah 2013 Collection kupitia Brand ya Mercedes Benz Tharaia Ahmed (wa tatu kushoto) sambamba na wadau wa tasnia ya urembo nchini wakati wa Onesho hilo. Wa nne kushoto ni Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 2004 Faraja Kotta (Mrs. Nyalandu), Nancy Sumari (Miss World Africa 2005) pamoja Mkurugenzi wa Mtandao wa Bongo5.com Lucas.

Jennifer Bash (katikati) akiwa na marafiki waki BBMika.

Wengine walikaa kwa nje kushuhudia 'Ally Rehmtullah 2013 Collection' kupitia Big Screen zilizofungwa kwenye bustani ya hoteli ya Serena (Zamani Sheraton, Royal Palm, Move n Pick) jijini Dar.
 
 Msanii mkongwe wa Muziki nchini Diva Karola Kinasha akitoa burudani kwa wageni waalikwa.
Mbunifu wa mavazi anayechipukia Jokate Mwegelo a.k.a Kidoti akizungumzia show ya 'Ally Rehmtullah 2013 Collection'.
 
Smiiiile (with my camera).
Designer Ally Rehmtullah, Super Model Fideline Iranga a.k.a Lady Gaga na Sinta a.k.a JLO wa Bongo.
Warembo walipendeza sana.
Ally Rehmtullah katika picha ya pamoja na Designer wenzake walioshuhudia Collection yake mpya ya Mwaka 2013.
Mrs. Faraja Nyalandu, Ally Rehmtullah, Nacy Sumari na Sinta wakishow love mbele ya Camera yetu.
Belvedere Vodka walitoa huduma za vinywaji vya aina zote kwa wageni waalikwa.
Moja kivutio kikubwa kwa wageni waalikwa kwenye "Ally Rehmtullah 2013 Collection" ni hili gari aina ya Mercedes Benz M CLASS yanayouzwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar es Salaam.Kwa picha zaidi Bofya hapa BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment