Friday, August 10, 2012

BACK FROM BBA-SOUTH AFRICA; PREZZOOOO:

Prezzo akiongea na waandishi wa habari juzi baada ya kufika kwao
Kenya akitokea Big Brother Africa South Africa.

Kama haufahamu ni kwamba Jaguar ambae kwa muda mrefu wamekua wakirushiana maneno kwenye media na Prezzo na kufanya watu waone wanabeef, aliweka tofauti zao pembeni na kumsupport sana Prezzo wakati akiwa BBA kwa kupiga kampeni watu wampigie kura ili ashinde.
Watu wengi walitamani kusikia Prezzo atasema nini kuhusu hiyo kampeni iliyofanywa na mtu ambae wanabeef (Jaguar).
Prezzo amesema “namshukuru kama alinisimamia kwa kiwango hicho, ukienda kwenye show kama hii kwa mfano unajua unakwenda kuwakilisha nchi yako so hata kama kuna uadui wowote mnaweka kando kwa sababu nchi yako ndio inajalisha kwa hiyo mambo mengine yote tunapuuzia mbali.
Jaguar.
Kwenye line nyingine President CMB amesema “napenda kusema asante kwa kunipigia kura nashkuru, na u know kama kawaida wakati wote tuko pamoja man binafsi unajua sina uhasama na mtu yeyote yule u know, maisha ni mafupi  unajua ukizidi kununa unapunguza maisha yako ukizidi kucheka unaongeza maisha yako, wakati wangu wa kucheka ndio huu na ntaendelea kucheka so ambao wananiona nikicheka chekeni na mimi”
Kuhusu uwezekano wa yeye kupiga kolabo na Jaguar baada ya kutangaza kwamba hana uhasama na mtu, CMB amesema “hiyo daraja tutavuka tukifikia, kwa sasa hivi yani bado kuna vitu vingi mi mwenyewe sijatulia hata vizuri, sijamaliza hata kutoa nguo zangu kwenye mabegi so tukifika kwenye hiyo daraja tutaivuka then wakati huo”

No comments:

Post a Comment