Wakali Dancer wakiwa na bendera yenye nembo yao wakati wakisherehekea miaka 4 ya kuanzishwa kundi lao.
Kundi la Wakali Dancers likishambulia jukwaa.
...wakizidi kunogesha sherehe hizo.
...wakicheza wimbo wa Thriller ulioimbwa na Michael Jackson.
...wakizidi kupagawisha.
Wanamuziki wa Kings Taarab wakiwa jukwaaani.
Maua Tego wa Coast Taarab akiwajibika.
Talent Band wakitoa burudani kwa mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka.
Wakali Dancers wakipongezwa.
Familia ya mmoja wa wasanii wa Wakali Dancers ikifuatilia onyesho hilo.
Kundi la Kidumbaki likitoa burudani.
Msanii anayefahamika kwa jina la Zimwi akitoa burudani.
Mpigapicha mahiri wa magazeti ya Global Publishers, Issa Mnally, akilishwa keki na shabiki wa burudani.
Mmoja wa wawakilishi wa Wakali Dancers akilishwa keki ya Jumapili.
SHEREHE za miaka minne ya kundi la Wakali Dancers jana zilifana ndani ya ukumbi wa kisasa wa burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar. Vikundi vya taarab vya Kings, Coast Modern na Kidumbaki kutoka Zanzibar pamoja na Talent Band vilifanya ‘bonge la kufuru’ kwa mashabiki waliofika katika ukumbi huo kwa ajili ya kuburudika wikiendi.PICHA ZOTE: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS/GPL
No comments:
Post a Comment