lililoandaliwa na kituo cha luninga cha EATV-
channel 5, ting'a kali namba moja kwa vijana,
Afrika mashariki. Shindano hili linafanyika
katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar-es-Salaam.
Washiriki ni lazima wawe na umri wa miaka 14-90
na wawe kwenye kikundi kisichopungua watu wanne na
wasiozidi sita Watapatikana washindi watano kutoka kila
wilaya ambao watashindana mpaka apatikane mshindi
mmoja atakayepewa zawadi ya shilingi millioni tano za
Tanzania. Leo ndo ilikuwa zamu ya wilaya ya Kinondoni
katika viwanja vya leaders club, kinondoni. Itahamia Don
Bosco-Upanga kwa wilaya Ilala na mwisho TCC-Chang'ombe,
kwa TMK-kiumeni. Pia matukio ya shindano hili
yatarushwa siku ya j'5 saa tatu na nusu usiku.
Smart group wakikamua...walichukua nafasi ya kwanza.
Black head from D.13 wakionesha uwezo wao....walichukua nafasi yapili.
G. Makoba wakiwa kikazi zaidi...walichukua nafasi ya tatu.
The best from kino waliingia na style yao ya baiskeli Walitisha kimtindo fulani...walichukua nafasi ya nne.
Wanaitwa Tatanisha group. Na kweli walitatanisha na style yao ya kanga moko. Hapa ni wakati wanajiandaa kuingia kwenye kinyang'anyiro...walichukuwa nafasi ya tano.
Majaji. Kutoka kushoto ni Super nyamwella. Katikati ni Lotus wa kipindi cha Nirvana cha EATV na Prince Dully Sykes.
Jaji namba moja...Lotus akiwa kazini.
Jaji namba mbili...Prince Dully Sykes akihukumu
Mamia ya mashabiki waliokusanyika kushuhudia Dance Mia Mia-leaders club...kinondoni.
'Wadhungu' nao hawakuwa nyuma...
Baadaye mashabiki wakataka majaji nao waoneshe kama kweli na wao wanajua ku-dance... sio kujifanya kuhukumu tu!
Majaji wakasimama kwenda kuonesha mauwezo yao.
Bas'sawa....kwenye moja na mbili DJ Sama kutoka All hits Station East Africa Radio akawagongea ngoma!
Jaji namba moja...Lotus, akaonesha kwanini yeye
ni jaji.
Mtoto Lotus aliendelea kuwapagawisha watazamaji.
Raia wali-salute kwa mtoto huyu wa kihaya.
...CHEZEA LOTUS WEWE!
Ikaja zamu ya jaji namba mbili...Dully. Akaingia na
mpira wa kikapu. Watu hawakukubali, wakaanza
kupiga kelele za bingili bingili bingili bingili bingili!
Akauliza nini...wakajibu 'bingili bingili bingili bingili'.
Akasema bas'sawa....akaanza kubingilika.
Raia wakaridhika...akaaga.
Halafu ndo akaja jaji namba tatu... Super Nyamwela. Akafunika mbaya.
Raia wakabadilisha maombi. Sasa wakataka ma-presenter wa Dance Mia Mia nao waoneshe kama wanajua!
Akaanza 'mtoto' barbz...akatisha
Saigon akasema mimi mtu wa mistari bwana...basi akakamua mbaya.
Bas'sawa.
No comments:
Post a Comment