Tuesday, April 24, 2012

"MAPENZI YA BBM" NEW TRACK BY DULLY SYKES:

Anajulikana kwa kuwa na tungo nyepesi lakini ambazo hukamata ndani ya muda mfupi na kwa aina yake. Utakumbuka enzi za Nyambizi na Julieta. Labda hicho ndicho anachotaka kukifanya mara hii kwa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Mapenzi Ya BBM akimaanisha Mapenzi ya kwenye App ya simu za Blackberry ya Blackberry Messenger(BBM).
Siku hizi Bongo BBM is a thing.Ukiwa huna BBM unaonekana kama namna gani vile.Watu hawaombani namba za simu bali wanaombana PIN.Ukienda kwenye shughuli usishangae kuona watu wamekaa meza moja lakini hawaongei.Kila mmoja yupo “bize” kwenye BBM akiteta na watu walio mbali na pale! Hili naliona la ajabu.
Wimbo ni kutoka Dhahabu Records ambayo ni studio inayomilikiwa naye Dully Sykes iliyopo kule Tabata jijini Dar-es-salaam.

No comments:

Post a Comment