Thursday, January 5, 2012

SKYNER; NATAMANI NITEMBEE MTUPU, NAUMIA SANA NA JOTO LA DAR:


MSANII mwenye umbo la utata katika tasnia ya filamu bongo Skyner Ally maarufu kama Skyner, amefunguka na kusema kuwa mwili wake ulivyo mnene unamfanya awe katika wakati mgumu huku muda mwingine anatamani kuvua nguo na atembee mtupu kutokana na joto lililopo kwa sasa jijini. Alisema mwili wake ni mnene hivyo mara nyingi amekuwa akishinda sehemu yeye ubaridi.

Skyner alisema hata hivyo analazimika kuvaa nguo zisizobana ili kuruhusu hewa iweze kufanya kazi vizuri ndani ya mwili wake kwani bila kufanya hivyo anaweza kuumia sana au kutoka vipele vya joto.

Skyner akiwa kwenye moja ya scenes za filamu ya ‘Second Wife’

“Siyo kwamba sipendi kuvaa nguo zinazobana lakini nashindwa kutokana na mwili wangu, mimi nguo zangu mara nyingi nazopendelea kuvaa ni magauni makubwa ambayo yanasaidia  kuwa huru wakati wote,” alisema.
Hata hivyo DarTalk lilimuuliza swali Skyner, kam hata wakati wa mtoko wa usiku huwa anavaa nguo hizo, ambapo alijibu kuwa kwa wakati wa usiku huwa anavaa vimini, ingawa suruari za kubana huwa anavaa mara moja moja sana.

No comments:

Post a Comment