Wednesday, December 14, 2011

MWANAHABARI MKONGWE, SEPTI SULEIMAN, AFARIKI DUNIA:

Marehemu Septi Suleiman amezikwa katika makaburi ya familia huko Mwera Kichokani leo.
Wananchi mbalimbali wakiwa wamebeba mwili wa aliekuwakatibu mtendaji wa Tume ya Utangazaji zanzibar na mwanahabari mkongwe Marehemu Septi Suleiman ambaye amezikwa huko kijijini kwao Mwera Kichokani.
Wananchi mabalimbali wakisali sala ya maiti ili kumuombea Marehemu Septi Suleiman aliefariki leo katika Hospitali ya mnazi mmoja huko Zanzibar.Picha Zote na Yusuph Simal,Maelezo-Zanzibar
----
Na Fatma Mzee Maelezo Zanzibar
Mamia ya wananchi wa Zanzibar wa Kike na Kiume leo asubuhi walishiriki katika mazishi ya mtangazaji mkongwe Septi Sulemein Juma aliezikwa kijijini kwao Mwera nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Mazishi hayo yalihuzuriwa na watangazaji mbalimbali wa Zanzibar pamoja na wakurungenzi wa vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo vya utangazaji na magezeti wakiongozwa na mkurugenzi wa habari maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda.

Marehemu Septi alianza kazi ya utangazaji mnamo mwaka 1964 katika idara ya habari na utangazaji katika semu ya Sauti ya Tanzania Zanzibar akiwa mtangazaji mwanafunzi .Baadae alikwenda China katika idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa kwa muda wa miaka mitatu.

Alirejea Zanzibar mnamo mwaka 1976 kuendelea na kazi katika Sauti ya Tanzania Zanzibar .Septi Suleiman baadae aliwacha kazi ya utangazaji na kujiunga na vyama vya wafanya kazi vya OTTU Tanzania.

Mnamo mwaka 1996 aliteuliwa kuwa Mkurungenzi wa Idara ya Sauti ya Tanzania Zanzibar katika mwenzi wa May ambapo kazi hiyo aliendelea nayo mpaka mwaka 2001 ambapo aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Alistaafu kazi katika mwaka 2006 ambapo baadae alifanya kazi akiwa Mkurugenzi wa redio ya Adhana Zanzibar mpaka kifo kilipo mtokea.
Marehemu Septi Suleiman Juma amefariki akiwa na umri wa miaka 69 na  ameacha mke na watoto 4.

No comments:

Post a Comment