Friday, November 4, 2011

SANGARA WACHANGA 900 WAKAMATWA WAKIPELEKWA KIWANDANI:

Kikosi cha doria cha Idara ya Uvuvi mkoani Mwanza, kimekamata zaidi ya samaki wachanga 900 aina ya Sangara kwenye gati la kufikishia samaki katika kKiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Vicfish kilichojengwa kandokando ya ufukwe wa Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Samaki hao ambao uzito wao haukufahamika mara moja wamekamatwa muda mfupi nbaada ya boti ya wakala anayesambazia kiwanda hicho samaki kutia nanga kwenye gati hilo.

Mkuu wa Kikosi cha Doria cha Idara ya Uvuvi mkoani Mwanza, Juma Makongoro pamoja naye Bwana Lukanga ambaye ni Mkuu wa Maabara ya Ubora wa Samaki iliyopo Nyegezi wamethibitisha kukamatwa kwa samaki hao wachanga kwenye gati la kufikishia samaki kiwandani hapo ambapo wanaaminika kuwa walikuwa ni kwaajili ya kuchakatwa.
Lukanga amesema kuwa samaki hao wamekamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kulikuwa na boti ambayo ilikuwa ikitoka kwenye moja wapo ya visiwa vilivyopo katika Ziwa Victoria kwa upande wa Tanzania ambayo ilikuwa imebeba shehena ya sangara wachanga kwa ajili ya kwenda kuwauza katika Kiwanda cha Vicfish jijini Mwanza usiku.

Taratibu zinafanyika ili kupata kibali kutoka mahakamani kwa ajili ya kugawa samaki hao kwa baadhi ya shule au taasisi zingine ambazo zinahitaji msaada wa chakula kwa vile samaki hao hawana madhara kiafya na kwamba hatua nyingine kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Nyavu haramu chanzo cha uvuvi samaki wasio na viwango.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Vickfish, Murtaza Alloo, amethibitisha samaki hao kukamatwa lakini amesema samaki hao bado walikuwa ni mali ya wakala kwa vile walikuwa hawajapokelewa kiwandani.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kwa kipindi ch miaka mitatu iliyapita viwanda vya kusindika minofi ya samaki vilivyoko eneo la Kanda ya Ziwa vimekabiliwa na uhaba wa samaki , hali ambayo imesababisha viwanda mbalimbali kupunguza wafanyakazi.

Samaki wasio ruhusiwa ni wale walio chini ya ukubwa wa sentimita 50.

No comments:

Post a Comment