Thursday, November 10, 2011

MWENYEKITI WA CHADEMA, MH FREEMAN MBOWE, ALIVYOJISALIMISHA JANA KATIKA OFISI ZA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA:

 Mwenyekiti wa chama cha demokrasi na maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akiwasili kwenye Ofisi za Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana asubuhi kwa ajili ya kujisalimisha kufuatiwa kusakwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kuvunja sheria.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiingia katika ofisi za mkoa za Jeshi la Polisi mkoni Arusha jana, aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Joyce Mukya akiwa amemsindikiza mwenyekiti wao kujisalimisha Polisi.

 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anatafakari jambo ndani ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha jana.
 Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, Saimon Pilo (kulia) akiwa amempokea Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe (katikati) katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanya nae Mazungumzo,wakati Mwenyekiti huyo alipofika Kituoni hapo Kujisalimisha jana asubuhi. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Joyce Mukya alieongozana na Mwenyekiti wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akitoka kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na kuelekea katika Ofisi ya Upelelezi Wilaya ambapo alielekezwa aende huko na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha. Picha zote na Woinde Shizza, Arusha.

No comments:

Post a Comment