Wednesday, November 2, 2011
MWANZA: MABOMU YALIPULIWA KUTAWANYA WAANDAMANAJI WA KESI YA KUCHOMWA KWA KITABU CHA QUR'AN:
Katika hali isiyotarajiwa, ghafla mazingira ya mahakama ya mwanzo iliyoko karibu na ofisi za idara ya maji safi na maji taka jijini Mwanza, eneo la Kemondo na maeneo ya Ghandh hall, Polisi wamelazimika kulipua mabomu ya machozi majira ya saa nne asubuhi ili kuwatawanya waandamanaji waliofurika kwa wingi nje ya mahakama ya Wilaya ya Nyamagana wakifanya vurugu kushinikiza maamuzi yafanyike dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo….
Hali tete ilianza kwa waandamanaji hao kufanya vurugu kwa madai ya kutaka waliopewa dhamana wasipewe dhamana, huku wengine wakisema hawataondoka mahakamani hapo pale tu watakapo kabidhiwa watuhumiwa hao...
Mzozo wa waandamanaji na askari wa jeshi la polisi.
HALI ILIVYOKUWA MARA BAADA YA DAKIKA 30:
Toka angani eneo la mahakama ya wilaya Nyamagana. Jumla ya watuhumiwa wanne wanadaiwa kushirikiana kuchoma Qur'an, asubuhi ya leo wamefikishwa mahakamani hapa kujibu mashtaka dhidi yao katika kesi inayotajwa kuahirishwa zaidi ya mara nne sasa kutokana na kuhofia usalama wa watuhumiwa.
Watuhumiwa wanaohusishwa na kesi hiyo ni waumini wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) ni Tumaini Jumanne (30) ambaye ni mwalimu wa Biblia, Petro Mashauri (29) mfanyabiashara, Dickson Magai (30) mfanyabiashara na mwanamke pekee, Kalista Mlomo ambaye ni mkulima.
Wakikabiliwa na mashitaka matano ambayo ni kula njama, kufanya kusanyiko lisilo halali, kuingia kwa jinai nyumbani kwa Husna Hamis na kuharibu mali, pamoja na lile linalozungumzwa zaidi la kudhalilisha dini kwa kuchoma moto kitabu cha Qur'an Tukufu.
Kesi imesababisha barabara kufungwa kwa muda hadi hali itakapo tulia.
Si biashara tena bali msaada kukosha macho kwa maji ya kahawa.
Askari wa jeshi la polisi wakifanya doria eneo la mahakama.
Kutokana na hatua ya kufunga barabara watu wamelazimika kutembea kwa miguu nao polisi wakipiga marufuku kusanyiko la aina yoyote kwenye eneo husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment