Sunday, October 2, 2011

TUSKER ALL STARS SHOW, NAIROBI KENYA:

Hivi ndivyo Wakazi wa la Nairobi na kwingineko walivyotapika ndani ya uwanja wa carnivo,ambako ndiko tamasha la Tusker All Stars 2011 lilikofanyika,ama kwa hakika ni tamasha ambalo limefana sana ndani yajiji hilo,pamoja na kuwepo na hali ya mvua m vua,lakini washabiki wa tamasha hilo ndio kwaanza walikuwa wakijiachia vilivyo uwanjani hapo huku wakipata vinywaji mbalimbali kutoka kampuni yaEABL-Kenya.Tamasha la Tusker All Stars 2011 limeratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions kwa kushirikiana na wadau wengine,huku wadhamini wakuu wa tamasha hilo ni Kampuni ya East African Breweries Ltd-Kenya kupitia kinywaji chake cha Tusker.

Ndani ya uwanja wa Carnivo jijin Nairobi,ilikuwa ni shangwee tuu.
Wanamuziki wa Kimataifa,Cabo Snoop kutoka nchini Angola pamoja na Eve E kutoka nchini Marekani wakijiachia vilivyo kwa pamoja jukwaani, huku mayowe na miluzi ikiwa imetawala kila kona ya uwanja.
Mmoja wa madada wakali katika miondoko ya hipo hop nchini Marekani,Eve E akiwaachia mistari wakazi wa Nairobi,ambao wengi wao walikuwawakivutiwa nae kwa namna ambavyo alikuwa akionesha kukomaa kwake kwenye anga ya muziki wa hip hop.
Mkali wa Reggae kutoka nchini Jamaica,Shaggy akiimba kwa hisia jukwaani.
Shaggy ni mmoja wa wanamuziki ambao kiukweli awapo jukwaani hanamasikhara kabisa na uwanja wake,kila wakati hupenda kuhakikisha watu wanashangweka tu,na ndivyo ilivyokuwa kwenye shoo yake usiku wa leo,kila wakati alikuwa akiwaimbisha mashabiki nao bila hiyana walikwenda nae sambamba,hali iliyomfurahisha zaidi.
Back voko wa Shaggy akifanya kweli.
Shaggy na bak voko wake wakilishambulia jukwaa,huku maelfu ya mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakipaga mayowe kuonesha kuwa wanakunwa vilivyo na umahiri wa wanamuziki hao.
Mmoja wa wasanii nyota wa Tusker All Stars 2011 kutoka nchini Rwanda,aitwaye Alpha akiwakuna vilivyo wakazi wa jiji la Nairobi na wimbo wake wa Nasonga mbele.
Mkali mwingine wa Tusker All Stars 2011,Davies kutoka nchini Uganda akilishambulia jukwaa vilivyo na madensa wake katika miondoko ya kindombolo ndombolo hivi.

No comments:

Post a Comment