Saturday, October 1, 2011

EVE E,SHAGGY NA CABO SNOOP WATAMBA KUFUNIKA TAMASHA LA TUSKER ALL STARS-KENYA:


Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Eve E akiwasili mapema jana asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya akiwa amepokelewa na mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd kutoka Tanzania, Bwana Balozi Kindamba (kushoto) na kulia ni mmoja wa wanausalama wa Eve E,Ujio wa Mwanamuziki huyo anaungana na wanamuziki wengine akiwemo Shaggy,Cabo Snoop pamoja na nyota wa Tusker All Stars, Peter Msechu, Davis pamoja na Alpha wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa moja baadae leo (jumamosi) kwenye viwanja vya Carnivo jijini Nairobi ndani ya tamasha la Tusker All Stars 2011.
 Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Shaggy akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari jijini Nairobi kuhusiana na Tamasha la Tusker All Statrs 2011 litakalofanyika leo jijini Nairobi, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya EABL-Kenya ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo.

 Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya EABL-Kenya ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo akizungumza na Waandishi wa habari juuu ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika loe.
 Baadhi ya wasaniii ambao watashiriki kwenye tamasha la Tusker all stars 2011 leo, Kutoka kushoto ni msaniii mahiri kutoka nchini kenya Amani na Jaguar mwingine ni Alpha.
Kulia ni Mmoja Kati ya Wakurugenzi wa Clouds Entertainment Ruge Mutahaba akiteta jambo na Mwanamuziki Mahiri kutoka nchini Marekani Shaggy jana asubuhi jijini Nairobi.
Mwanamuziki Mashuhuri kutoka Nchini Marekani Eve E akitia saini kwenye bango lenye tangazo jipya la Kampeni Kutoka East Afrika Breweries la '' Unywaji Pombe Kistaarabu ama Responsible drinking.
Eve E na Alpha.
Kama kawa yoo.

Baadhi ya wanamuziki waliojitokeza kuunga mkono kampeni Mpya ya EABL-Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanamuziki Mahiri kutoka nchini Marekani Eve E (Wa Pili Kushoto) na Kwanzia Kulia ni Shanggy,Cabo Snoop,Msechu na Davies.

No comments:

Post a Comment