Monday, August 15, 2011

MSAMA AUCTION MART YAKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII PAMOJA NA MITAMBO YA KURUDUFU KAZI HIZO:

Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye kituo cha polisi Urafiki mara baada ya kuwanasa watuhumiwa wa kurudufu kazi za wasanii mbalimbali, aliwataja watuhumiwa hao ni Bashiri Abdul na Jofrey Anatori (Wakazi wa mabibo jijini Dar es salaam). Aidha, Msama alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo ya Mabibo mpakani jijini Dar wakiwa na mitambo yao pamoja na kazi walizozirudufu zenye thamani ya Tsh milioni 25.
Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama, akionesha baadhi ya kazi feki zilizorudifiwa na watuhumiwa hao.
Mmoja wa watuhumiwa akiwa na vifaa vyake vya kurudufia pamoja na kazi alizokwisha zirudufu tayari kwa kuzipeleka sokoni.
Baadhi ya kazi feki zilizokamatwa na kampuni ya Msama Auction Mart maeneo ya mabibo mpakani jijini Dar.

No comments:

Post a Comment