Tuesday, August 30, 2011

LOVENESS FLAVIAN NDIYE MISS VODACOM SPORTS LADY:

Loveness Flavian akiwa katika pozi la picha baada ya kushinda taji hilo na kuwa mrembo wa 3 kati ya warembo 15 watakaoingia nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania zitakazofanyika September 10 2011, jijini Dar es salaam.
Miss Vodacom Sports Lady, Loveness, akipongezwa na warembo wenzake waliofanikiwa kuingia tano bora ya kuwania taji hilo la michezo.
 
Warembo wa Vodacom miss Tanzania waliofanikiwa kuingia tano bora ya miss Vodacom Sports Lady kabla ya kutangazwa kwa mshindi. Kutoka kushoto ni Rose Hubert, Husna Maulid, Loveness Flavian, Salha Izrael, na Delillah Ghalib.
 
Vodacom Miss Top Model, Mwajab Juma (Katikati), ndiye alikuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 akiwa na mshindi wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora, Vodacom Miss Photogenic, Tracy Mabula (Kushoto) wote wakiwa na mwenzao watatu kuingia hatua hiyo, Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian (Kulia).

No comments:

Post a Comment