Sunday, July 31, 2011

TAQWA SECONDARY, MABINGWA WA AIRTEL RISING STAR - MWANZA:

Mabingwa, Taqwa Secondary.
Nsumba Secondary.
Fainali ya Airtel Rising Star imefanyika jana jioni kwenye kituo cha mwanza viwanja vya Buswelu Sekondari ambapo kulikuwa na michezo miwili, mchezo wa kwanza umeshuhudia Mwanza Sekondari wakiibuka nafasi ya tatu mara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Buswelu sekondari goli likipatikana kwa njia ya penati, mfungaji akiwa ni Selemani Ibrahimu, aliyefanikiwa kumhadaa kwa ufundi kipa wa timu pinzani.

Mchezo wa pili wa fainali ulikuwa ni kati ya Nsumba Sekondari na Taqwa kipute kilichoanza kwa kasi ya ajabu na ushindani mkubwa lakini hadi dakika za kawaida za mchezo zinamalizika ngoma droo 0-0 ndipo ikaamuliwa njia ya matuta iliipa ushindi Taqwa kwa penati 4-3, penati zilipigwa nane, nane.

No comments:

Post a Comment