Wednesday, July 13, 2011

MGOMO WA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA COCACOLA KWANZA JIJINI DAR ES SALAAM UNAVYOONEKANA PICHANI:


Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha soda cha Coca Cola Kwanza, kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mgomo wao juzi asubuhi. Wafanyakazi hao waligoma wakishinikiza uongozi wa Kiwanda hicho uwaongezee mishahara.
Baadhi ya wafanyakazi wakiongea na waandishi wa habari.

Kiongozi wa TUICO alifika kuwatuliza wafanyakazi hao na kuahidi kuzungumza na Menejimenti ya Kiwanda hicho.Mpaka  majira ya saa sita mchana juzi,mgomo ulikuwa unaendelea na Uongozi wa kiwanda hicho ulikataa kuzungumza chochote na waandishi wa habari.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment