Wednesday, July 6, 2011

CHUPU CHUPU AUWAWE BAADA YA KUPIGWA KWA CHUPA NA SHEMEJI YAKE:

 Dereva John Gwau akiwa amelazwa katika wodi na.4 katika hospitali ya mkoa wa Singida akiendelea kupata matibabu baada ya kupigwa na shemeji yake Celestin Mgoo kwa tuhuma za kufuliwa nguo na dada yake Ruth.

Dereva wa kampuni ya usafirishaji ya ‘Rich On’ ya jijini Dar-es-salaam John Gwau (35) amenusurika kuuawa na shemeji yake baada ya kupigwa vibaya kichwani na chupa ya bia.
Akizungumza  kwa taabu  akiwa amelazwa wodi namba nne katika hospitali ya mkoa,Gwau amesema alikumbana na dhahama hiyo julai nne mwaka huu saa sita usiku eneo la Mughanga mjini humo.

Amesema mapema siku hiyo ya tukio,shemeji yake Celistin Mgoo ambaye ametengana na dada yake anayeitwa Ruth,alimgombeza Ruth kwa kitendo chake cha kufua nguo zake (Gwau).
Dereva huyo amesema Ruth alimjibu Celistin kuwa haoni kosa lo lote kwa kitendo cha kufua nguo za kaka yake Gwau ambaye kwa wakati huo,alikuwa mgonjwa.
“Majibu hayo na kitendo cha dada kufua nguo zangu,vilimuudhi shemeji ambaye usiku huo alinijia chumbani kwangu akiwa na chupa tano za bia kwa lengo la kuzitumia kunipiga”alisema.
Gwau amesema baada ya kuingia chumbani, alimpiga kichwani na chupa ya bia na kupelekea aanguke chini na kuzirai na kuzinduka kesho yake mchana.Baada ya kuzirai,mtuhumiwa alitumia chupa hiyo iliyopasuka kwa kumcharaga sehemu mbalimbali za uso.

“Dada yangu Ruth ambaye ni mwalimu katika shule ya msingi Mughanga na ndugu yangu Athumani Rajabu,baada ya kuniona natokwa damu nyingi huku nikiwa nimezirai,wote wawili walianguka chini na kuzirai.Wote  wamelazwa hapa hospitali ya mkoa”alisema Gwau.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Celina Kaluba,amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa Celestin amepandishwa kizimbani  Julai5 ,2011) kujibu tuhuma inayomkabili.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment