Thursday, December 1, 2011

JOHN MNYIKA: JITOKEZE KESHO 2ND DEC, 2011 KUKATAA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME

Mheshimiwa John Mnyika,Mbunge wa Jimbo la Ubungo(CHADEMA)na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
--
Kesho tarehe 2 Disemba 2011 katika Ukumbi wa Makumbusho Dar es salaam (mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM) kuanzia saa 4 asubuhi, EWURA imeitisha Mkutano wa Wadau kujadili ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa 155%(zaidi ya mara tatu ya bei ya sasa).
Nawaomba wanamtandao wote tuhamasishe umma kwa kutumia TEHAMA (sms, facebook, twitter, email na njia nyingine) ili wananchi waweze kuhudhuria mkutano husika kwa wingi na kutoa maoni.Kusoma Zaidi Bofya na Endelea......>>>>>>

No comments:

Post a Comment