Saturday, November 26, 2011

TEDY KALONGA; INTRODUCING MALAIKA HAIGHT:

Bila shaka unamkumbuka vyema Teddy Kalonga.Kama bado bila shaka unaweza kuitazama hiyo picha hapo juu na kuvuta au kufufua kumbukumbu yako.Kwa msaada tu(just in case) Teddy Kalonga au TK kama ambavyo wengi hupenda kumuita,aliwahi kuwa mtangazaji wa TV hapa nchini kabla ya kuelekea nchini Marekani anapoishi hivi sasa.TK pia ni mlimbwende au mwanamitindo.
Hivi karibuni TK alijivisha cheo kingine.Anaitwa Mama Malaika.Pichani juu ni TK,mumewe na mtoto Malaika Haight.Kwa mujibu wa blog ya TK ambayo unaweza kuitembelea kwa kubonyeza hapa, hii ni picha ya kwanza ya kumtambulisha rasmi mtoto Malaika.
Photo:Courtesy TK

No comments:

Post a Comment