![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg0KpAtD_GNBO7xj0EWrH446yEaTJp8MYihlU0pAueKwoXC8H0xP7FRLGD9ZUA2w92JXw4n0DSiNMEmonNet-MQWQRAjr9RRc4Fu5KfexcrKv-4c2YJzoR6PdcVsDcXdXkHQhO9jwrsEVh/s400/Stephen+Magaigwa.jpg)
Amesema kuwa Kupitia marekebisho ya katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar ya mwaka 1984 tangu nchi hizi mbili zilipoungana kuna mambo walikubaliana kwamba haya ni ya Muungano lakini yamekiukwa kupitia marekebisho ya katiba ya Zanzibar yaliyofanywa.
"Baada ya kutumia taaluma yangu kifungu baada ya kifungu nimegundua kuwa marekebisho hayo yameingilia mambo ya Muungano na kuleta mkinzano au mkanganyiko katika shughuli za kila siku za utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".
"Nilitegemea kuwa wanasheria wa serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wangechukuwa hatua maalum kurekebisha hali hii tangu awali kabla ya kuipeleka katika utekelezaji lakini walikaa kimya kama wataalamu wa sheria wasiojuwa kazi yao.
Mambo manne aliyogundua"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2GnwGLADAxIPVW4dp1a9ygdWccoXN6WBQFWAOEEwpnkD5izc9l4VFD642OIwxpTaNu5LsXwJn4Ud9iQgktHqLPs_3CiL87WEvwpwZZHiQhncx51DQ02yJmTe0ehQp6czGX1rHxB98AYrq/s400/Stephen+Magaigwa+3.jpg)
1.Haki za binadamu:- "Katika marekebisho ya katiba ya Zanzibar suala la Haki za Binadamu, katiba hiyo imezuia kwamba haliwezi kuja katika Mahakama ya Rufaa –Wakati Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jedwali la 1 unagundua kuwa suala la Mahakama ya Rufaa ni suala la Muungano"
"Lakini Haitoshi linapokuja suala la haki za binadamu nchi inayohusika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSL_xXUhJR1xYfAKoDE0pvfFDJmFCd7X6pPSZiWbbWudeNV9n4gDfcwqTlTN00RYg3pa9iVQv_2TDY_SRPQU69Geo9aSL4DxWJEqSNNed0uYZ8bzOAs-ydiDBHEq-5A3SQS23k6f4MBAXs/s400/Stephen+Magaigwa+2.jpg)
3.Majeshi ya Ulinzi:- "Katiba ya Jamhuri inasema kuwa nchi pekee ambayo imepewa mamlaka ya kuunda majeshi ya ulinzi au vikosi vya aina yeyote ile ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini Marekebisho ya kumi ya sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya katiba ya Zanzibar yanasema sasa wanaweza kuunda vikosi kama KMKM na kadhalika … Swali ni nani Amri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo? Kwani yanapoundwa lazima yawe na mtoa amri wake mkuu"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd1W-kYIQGJAuGueb5H963Mcx0nigyHaZuQeKabsDmUiy-Dn3q6qC3S3eESDgzQOnBuOmJWPMD4bzGfqKIRJbpnSEsFVprCxofmxO5N_R7TGzoDx89FjPUGgWlyx5FquMNjcMb1JcKtAgh/s400/Stephen+Magaigwa+4.jpg)
4.Wakuu wa nchi wawili:- "Ukisoma katiba ya Zanzibar 26(1) na ile ya Muungano kifungu cha 33(2) utagundua kuwa sasa tuna wakuu wa nchi wawili, sasa tunapokuwa na wakuu wawili ili hali katika katiba hatuna ruksa ya kuwa na ‘two head of state in one country’ hali hii inamaanisha nini?"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZmlgzzunSFVVL0X-5T5S_GFvnZvLYkCiMqCbtUNTdR1VeM6JFZbodLVaNprmzVQ2ALiKsPV7xu5THLAqo8QW9Ds6WNdmSgIE-483LV2RJPrBrF1UaIhCLnQH2AObRPiCL4bf80oeRdNhI/s400/Stephen+Magaigwa+1.jpg)
Lengo kuu:- Nitaomba Mahakama hiyo iamuru katiba ya Zanzibar irekebishwe kuondoa kasoro hizo haraka iwezekanavyo ili kuleta sifa ya Muungano.
"Lakini Haitoshi linapokuja suala la haki za binadamu nchi inayohusika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
ReplyDeletebest hotel in tanzania
Mwanasheria toka Mwanza umekumbuka jambo la msingi sana hususani kipindi hichi tunachoelekea kwenye upatikanaji wa katiba mpya.
ReplyDelete