

Harusi ya muigizaji maarufu wa Nigeria MERCY JOHNSON OZIOMA na mumewe PRINCE ODIANOSEN OKOJIE iliyofungwa jumamosi iliyopita katika kanisa la CHRIST EMBASSY jijini Lagos ilifana sana na kuhudhuriwa na mastaa wengi wa Nollywood hivyo kuvunja rekodi. Kabla ya harusi hii kufungwa kulikuwa na mgogoro mkubwa kati ya mke wa zamani wa PRINCE ODIANOSEN ajulikanae kama LOVELYNE OKOJIE aliyetoa pingamizi kuwa alishaolewa na hajaachwa pia amezaa nae watoto wawili na picha zao akatoa,lakini mambo yaliwekwa sawa na harusi ikafungwa vizuri tu.

Meeercyyyyy.

Aaanameremeta, anameremeta,bibi harusi anameremeta......, ana wakawaka...!!

Jim Ike(kushoto) na Keneth Okonkwo.
Stephanie Okereke akiingia ukumbini.
Kushoto ni muigizaji EMEKA IKE akiingia na kulia ni muigizaji wa Ghana Michel Majid wote walikuepo.
Msanii 2shots(kushoto)akiwa na muigizaji Mike Ezuruonye harusini.
Muigizaji wa Ghana Yvone Nelson(kushoto),Waje na Empress Njamah(Nollywood).
Comediana mfupi Nollywood Chinedu Ikedieze na mchekeshaji wa jukwaani AY.
Bonge ya keki, basi baadae sana...
No comments:
Post a Comment