Saturday, July 14, 2012

TAARIFA YA TANESCO JUU YA KUKATIKA KWA UMEME, MWANZA NA MBEYA:


Mwanza.
Mtu wangu wa 87.8 Mbeya au 88.1 Mwanza Kama siku yako imekua mbaya leo au siku nyingine mbili zilizopita kwa sababu tu ya kukosekana kwa umeme, najua mpaka sasa utakua hujafahamu kinachoendelea, na swali kubwa ninaloamini unahitaji kusikia jibu lake ni kuhusu chanzo cha kukosekana kwa huo umeme ambao wengi wanaamini ni mgao umeanza tena.
Tanesco imesema hakuna mgao wowote unaoendelea kwa sasa isipokua ni tatizo la kiufundi ambalo lilitokea ghafla na tayari mafundi wameshaanza kulifanyia kazi na umeme unaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Afisa Uhusiano Badra Masoud amesema hawezi kuahidi ni ndani ya muda gani tatizo litakwisha kabisa kwa sababu mambo ya ufundi hayatabiriki lakini kazi kubwa inafanyika kuhakikisha hali ya kawaida inarudishwa haraka.

No comments:

Post a Comment