Sunday, June 10, 2012

ONLY ONCE IN MY LIFE TIME WHEN I MET THE DECEASED BONGO SUPER STAR 'STEVEN CHARLES KANUMBA' @ CCM KIRUMBA-MWANZA:

Kumbukumbu nzuri ya picha nilizonazo katika maktaba yangu ni pamoja na picha nilizozipiga siku ya jumapili tarehe 22 May 2011 katika uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza ambapo mechi ya hisani kati ya Bongo Movie Club na Mwanza All Stars ilichezwa na hatimaye Bongo Movie Club kuibuka na ushindi wa goli 1-0. Miongoni mwa wasanii/waigizaji wakubwa nchini walioshiriki pambano hilo ni pamoja na Vincent Kigosi-Ray, Jimmy Mponda-JPlus, Jenifer Kyaka-Odama, Wema Sepetu, Mwanaidi Suka-Mainda, Jacob Steven-JB, Single Mtambalike-Richie, Hisani Muya-Tino, Benson Kinyaiya-Ben, Mayassa Mrisho-Maya, Steve Nyerere na marehemu Steven Charles Kanumba (R.I.P) na wengine wengi. Binafsi, siku hii ilikuwa siku yangu ya kwanza na ya mwisho kuonana uso kwa uso na kuzungumza naye machache kuhusiana na filamu za hapa nyumbani Tanzania, ndugu yetu, aliyekuwa kipenzi cha wengi kati ya wale waliopenda kutazama filamu za Tanzania, marehemu Steven Charles Kanumba.
Ufuatao chini ni ukumbusho wa picha chache kati ya nyingi ambazo nilizipiga siku ile pale CCM-Kirumba zikimwonesha marehemu Kanumba jinsi alivyokuwa akijichanganya na mastaa wenzake wa Movie. Fuatilia:
Basi lililokuwa limewabeba wasanii wa Bongo Movie akiwemo pia marehemu Steven Kanumba likiingia uwanjani huku likizongwa na watu kibaooo.
 Watu wakikata tiketi za kuingia ndani uwanja kuweza kushuhudia mechi kati ya Bongo Movie na Mwanza All Stars.
 Gari likiingia ndani ya uwanja.
 Richie (Kushoto) na Tino wakiwasalimia wana Mwanza.
 JB akitroti kuelekea uwanjani.
Jalamba likaanza. Marehemu Steven Kanumba (Wasaba kutoka kushoto)
 Marehemu Kanumba katikati akifanya mazoezi ya viungo.
 Swahiba wake Ray, Richie, Tafu na marehemu Kanumba (Jezi nambari 11).
 Nambari 11, ndiyo ilikuwa jezi ya marehemu Steven Kanumba.
 Waweza mtafuta mwenyewe utamwona tu katikati humo.

 Richie akisogelea mpira.
 Ray nae alikuwepo.
 Ben na Claud 112.

 R.I.P braza.
 Kikosi kizima cha Bongo Movie.
 Na wanawake waliokuja nao.
 Tabasaaamu, limeshapotea.


 Benchi la Mwanza All Stars.
 Bongo Movie wakishangilia goli lao ambalo lilifungwa na Ray.
Half time
 Bibie Wema Sepetu naye akijishebedua.
 Nakumbuka hapa tulimzinga wapiga picha wengi kila mtu akitaka picha yake.
 Mwamjua huyu..? Anaitwa Mwanaidi Suka a.k.a Mainda.
 Shosti huyooo, Amber Rose wa Bongo, Wolper.

 Mayasa Mrisho 'Maya', Amber Rose 'Wolper' Masawe, Jack Pentzel (Jack Chuzi), Cathy
 Maua ya Bongo Movie yakicheza cheza.
 Baada ya hapo, kama kawa. Nikairudia 'desktop' yangu na kuzitupia clips zote kutoka maeneo yale ya CCM-Kirumba
 Ze DressCode, Caris haapaaaaaaaa, hiyo ndiyo ilikuwa dress code yangu ya siku ile. Pendeza eeh..!?

1 comment: