Thursday, May 31, 2012

HATA KAMA TUTAPAKI BASI EURO 2012,POWA TU!

Beki wa England,Gary Cahill, amesema hata kama timu yake itatumia style ya kupaki basi kwenye michuano ya Euro 2012 yeye kwake ni pouwa tu, kitu cha msingi ni kupata matokeo wanayoyahitaji. Beki huyo ambaye anachezea Chelsea, ametolea mfano mechi za klabu hiyo ya darajani dhidi ya FC Barcelona. Alisema, "Tulipaki basi dhidi ya Barca tukawatoa, tukapaki basi dhidi ya Bayern Munich tukawafungaa. Sasa sisi ni mabingwa wa Ulaya na historia itabaki hivyo miaka yote kwamba sisi ni mabingwa wa Ulaya 2012. Kwa hiyo hata England kama itatakiwa kupaki basi itakuwa powa tu mradi hiyo itusaidie kutwaa ubingwa wa EURO 2012 na baada ya hapo watu watasema England ni mabingwa wa EURO 2012 na wala sio mabingwa wa kupaki basi."

No comments:

Post a Comment