Friday, February 10, 2012

POSTER YA MOVIE YA 'KIJIJI CHA TAMBUA HAKI':



Kanumba akionesha kwa waandishi wa habari picha ya kwenye Cover ya movie mpya kutoka kampuni ya Kanumba The Great Films. Movie hiyo inayokwenda kwa jina la 'Kijiji Cha Tambua Haki' imedhaminiwa na Policy Forum na inategemewa kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment Limited.
'Ni filamu ya kipekee hakuna mapenzi humo, hakuna majumba ya kifahari wala suti nzuri, ni maisha halisi anayoishi Mtanzania wa leo kijijini'. Alisema Kanumba. Pia aliongeza kwa kusema kuwa filamu hii inatarajia kutoka mwishoni mwa mwezi huu (February) na imeshirikisha watu (wasanii/waigizaji) zaidi ya 400. Kaaazi kwenu wadau.

No comments:

Post a Comment