Thursday, October 6, 2011

SHUKRANI KUTOKA KWA DADA JOYCE SHAYO:

DSCN0012.JPG

S H U K R A N I

Kwa niaba yangu Binafsi, Mume wangu mpendwa JAMES na familia ya Mzee Phocus Shayo, napenda kutoa shukrani zangu za dhati na upendo kwa wafanyakazi wote wa BOT Tawi la Mwanza, Chuo cha BOT na wachache wengine walioko matawi mengine ya BOT kwa jinsi mlivyofanikisha sherehe zangu zote za harusi yangu kwa hali na mali.  Sina cha kuwalipa ila mwenyezi Mungu mwingi wa Huruma na Rehema, awarudishie kile mlichokitoa kwangu.

Nitakuwa mnyimi wa fadhila kama sitawashukuru makundi yafuatayo: -

1.   Wanakamati wote walioshiriki maandalizi ya sherehe za Kitchen na Send-off.
2.  Wafanyakazi walioshiriki harusi yangu Dar es Salaam.
3.  Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu kwa niaba ya Mwajiri kwa kunipa ukumbi nilioutumia wakati wa Send-off.
4.  Viongozi wote wa Tawi na Chuo kwa kujumuika kwa wingi katika sherehe zangu.
5.  Mwisho, wafanyakazi wa Tawi la Mwanza (wakiongozwa na viongozi wa Mfuko wa jamii), Wafanyakazi wa Idara ya Huduma za Kibenki na wote waliotuletea Zawadi nawashukuru wote.

“MUNGU AWABARIKI SANA”

JOYCE P. SHAYO.

No comments:

Post a Comment