Thursday, October 6, 2011

BOMOA BOMOA YA MTAA WA GHANA - MWANZA:


Zaidi ya kaya 80 katika Mtaa wa Ghana jijini Mwanza hazina mahali pa kuishi kutokana na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza juzi majira ya saa 3 asubuhi kubomoa nyumba walizokuwa wanaishi ili kupisha ujenzi wa mradi wa Jengo la Machinga Complex.



Wengine wakifanya mikakati ya hamahama.
Kwaheri mjengo...
Vibaka nao wamekuwa wakipitia mabati na mengineyo..

Hapa alikuwa akiishi balozi.
Wengine wakifanya mikakati ya hamahama.
Wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia maturubai kwa ajili ya kujisitiri wakati wakiwa katika harakati ya kutafuta sehemu nyingine ya kupanga.

Kutokana na bomoa bomoa inayoendelea Eneo la Ghana kwa sasa limekatiwa umeme hali inayosababisha ulinzi wa mali kuwa mgumu, usiku mzima wananchi hao wamekesha kulinda mali zao kwani vibaka walikuwa wakilandalanda kuiba mali zilizonje ya magofu ya nyumba zilizobomolewa sambamba na kung’oa flemu za milango na madirisha.
Huduma za maji tayari zimekwisha sitishwa.
Watoto hawana habari wanacheza kiduku tu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Wilson Kabwe amesema kuwa tayari notisi ya kuhama wakazi hao aliowaita kuwa ni wavamizi ilikwishatolewa kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kwamba kilichokuwa kinasubiriwa ni wao kuhama bila ya kubughudhiwa lakini wakakaidi agizo mpaka bomoabomoa ilipowakuta.


Kabwe, ameongeza kuwa tayari usanifu wa mchoro kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Machinga ulikwishafanyika na soko hilo linajengwa katika eneo hilo la Mtaa wa Ghana, Wilaya ya Ilemela.

1 comment:

  1. jamani walala hoi wenzangu wakati mwingine muwe mnatii sheria maana hii serikali siku zijazo inaweza kutumia hata mabomu kuwahamisha kwa nguvu maana hata mabomu hayajatengenezwa kwa wanyama.

    ReplyDelete