Thursday, June 30, 2011

SHEREHE YA KUMUAGA RAMSEY NOUAH PARADISE CITY HOTEL:

 Ramsey na Kanumba wakiingia sehemu ya tukio.
Baada ya shughuli nzima ya kushoot movie yao iliyobatizwa jina la Devil Kingdom kukamilika, Ramsey Nouah na mwenyeji wake Steven Kanumba walijumuika katika hafla fupi ya kumuaga nguli huyo wa movie nchini Nigeria iliyofanyika katika hoteli ya Paradise City iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam, maeneo ya Posta.
 Mkurugenzi wa Paradise City Hotel akisalimiana na Ramsey.
 Ramsey na Patcho Mwamba.

 Mkurugenzi wa Paradise City Hotel akitoa mawaidha yake ya kutaka umoja endelevu wa Movie Industry Afrika.
 Zamu ya Ramsey kuongea; alisema, Ipo siku kabla sijafa tutakuwa na movie industry yetu ya Afrika, Afrowood. Ipo siku mastaa wote wa movie Afrika tutafanya movie moja ingawa kwa sasa katika Afrika nchi zinazojulikana sana kwenye tasnia hii ni Nigeria, Ghana na Tanzania. 
 Kanumba nae alitoa yake ya moyoni kuhusu Industry hiyo, kwamba, kuna haja kubwa ya kuiendeleza fani hii kwa hali na mali ili hata watoto wetu wanaokuja nyuma wawe na urithi wa kujivunia katika movie, hata kama tusipokuwepo lakini historia itabakia.
 Picha ya pamoja ya wasanii wa movie na wadau wa Bongo movies.

No comments:

Post a Comment