Thursday, May 3, 2012

HARAMBEE YA WIMBO MAALUMU UNAOITWA 'MBONI YANGU' KWA AJILI YA KUCHANGISHA PESA ZITAKAZOMSAIDIA MWIGIZAJI 'JUMA KILOWOKO' a.k.a SAJUKI KWENDA KUTIBIWA INDIA:

Jana (juzi) kuanzia mida ya saa mbili usku, wasanii mbalimbali pamoja na baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania walikutana kwa ajili ya kurekodi  wimbo utakaoitwa mboni yangu.

Wimbo ulianza kurekodiwa rasmi saa tatu kamili usiku.
Kutoka kushoto ni Dina Marios, Mh. Ester Bulaya mbunge wa viti maalum - vijana na Asma Makau.
Producer Tuddy Thomas, 'mpishi' wa wimbo huo kabla ya zoezi la uingizaji wa vocal.
Mh.Easter Bulaya akitia sauti yake pale.
Mh.Vicky Kamata nae aliwasili usiku huo kushiriki.
Mh.Vicky Kamata,Tudy, Ruge.
Kabla hajawa mbunge unakumbuka alishawahi kufanya kazi kadhaa za mziki. Anakumbuka enzi katika wimbo huu.
Mwana FA.
Ali Kiba for Real.
Mzee Yusuph akiandika msahairi yake, pembeni ni Peter Msechu.
Juu Mzee Yusuph akiweka sauti yake.
Zamu ya Ali Kiba ikafika.
Tasnia ya Bongo movie iliwakilishwa na Wema Sepetu.....

Pamoja na William Mtitu hawa ni wasanii ambao ukiwaita kwa lolote wapo radhi hata kama ni usiku wa manane.
Madee akipitia mashairi yake.
Kimodo na Barnaba.
Ditto.
Madee akirekodi sauti.

Ditto, Amini na Afande Sele.
Zamu ya Amini.
Peter Msechu
Profesa Jay akiandika mistari yake.
Afande Sele nae akiandaa mistari yake.


Fid Q hakubaki nyuma.

Ndugu Juma Kilowoko almaarufu 'Sajuki', jinsi alivyo kwa sasa.
Kusema kweli ndugu yetu anaumwa, tumsaidieni.

Wimbo huu unaitwa MBONI YANGU ukiwa ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambaye anahitaji mchango wako wa hali na mali kuokoa maisha yake. Awali, sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali hii aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili. Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwaajili ya kupata matibabu. Wimbo uliokuwa ukirekodiwa unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe (Wastara) aliyoiita MBONI YANGU na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo ukiiimbwa na Wastara (Mkewe). Wimbo huu umerekodiwa maalumu kwa lengo la kuhamasisha kuchangia pesa zitakazotumika kama gharama ya matibabu yake na utaanza kusikika kesho Clouds Fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana Clouds Tv. Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili, Sajuki anaumwa sana.

Wimbo huu ulirekodiwa mpaka mishale ya saa tisa kasoro usiku, Dina Marios ilibidi alale kidogo kwa kuwa  alikuwa anasinzia ila mapema saa kumi na mbili leo alfajiri alikuwa macho tayari kwa kujiandaa na "LEO TENA". 
NB: Kuchangia, tuma msaada wako (pesa) kupitia namba ya tigo pesa ya mkewe Wastara: 0713666113 au M-Pesa:0762189592

Special Thanks to:
Coordinators: Ruge Mutahaba & Dina Marios,
Director:         Mwasiti Almasi,

Producer:        Tuddy Thomas.

No comments:

Post a Comment