Tuesday, November 29, 2011

TAMASHA LA STREET UNIVERSITY LAWEKA HISTORIA ARUSHA:

Eric Shigongo akitoa mada za ujasiriamali na namna ya kujikomboa na umaskini kupitia biashara.
Msanii wa muziuki wa injili, Pastor Wambura wa Arusha akifanya vitu vyake jukwaani.
 James Mwang’amba akitoa mada za ujasiriamali na namna ya kujikomboa na umaskini kupitia biashara.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege na Christina Shusho wakitoa burudani jukwaani kwenye tamasha hilo.
Wasanii wa kundi la muziki wa injili la Dot Com Generation wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mtoa mada mkuu katika tamasha hilo, Eric Shigongo akibadilishana mawazo na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema wakati wa tamasha hilo.
Mratibu wa Tamasha hilo, James Mwang’amba, (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini -Chadema Mheshmiwa Godbless Lema.
Msani wa muziki wa kizazi kipya, Abass Kinzasa ‘20%’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha hilo.
Sehemu ya umati uliohudhuria tamasha hilo.
  --
Tamasha kubwa la ujasiriamali la Street University lililofanyika kwa kishindo ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumapili iliyopita, limeweka rekodi kwa kulifanya jiji hilo litingishike kwa burudani kabambe kutoka kwa wasanii kibao walio kamua jukwaani pamoja
na mada motomoto za ujasiriamali zilizotolewa.

Risasi mchanganyiko lilikuwepo kwenye uwanja huo na kushuhudia jinsi umati uliofurika, wakiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema na askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie walivyoyafurahia mafunzo ya ujasiriamali na burudani ya kukata na shoka iliyoporomoshwa na wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina
Shusho, Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’ , Glorious Singers, Dot Com Generation na Pastor Wambura.

“Tumepata mwitikio mkubwa kuliko hata tuliuvyotegemea. Tunawashukuru sana wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kwa kutuunga mkono nakujitokeza kwa wingi kusikiliza tulichowaandalia. Tunaamini maisha ya wengi yatabadilika kwani tumepandikiza mbegu za ushindi na mafanikio maishani.

“Tunawashukuru sana wadhamini waliowezesha kufanyika kwa tamasha letu, Kampuni ya Global Publishers Ltd, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple ARadio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM),Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM)  na Radio 5 (105.7FM), zote za jijini Arusha,” alisema Mwang’amba ambaye ndiye aliyekuwa mratibu watamasha hilo.

No comments:

Post a Comment