Tuesday, November 29, 2011

SOKO JINGINE JIJINI MBEYA LAWAKA MOTO JANA:

Baadhi ya wafanyabiashara na wakazi wa maeneo ya jirani na soko kuu la mji wa Tunduma jijini Mbeya wakishuhudia moto mkali uliokuwa ukiteketeza soko lao hilo hapo jana. Moto huo ambao unadaiwa ulianza kidogo kidogo na baadae kuwa mkubwa, ulianza majira ya saa 11 jioni ya jana. Taratibu za awali za kuuzima moto huo zilichukuliwa lakini hakukuwa na mafanikio yoyote na baadae walifika askari wa kikosi cha zimamoto cha mkoa wa Mbeya wakiwa na magari yao ambayo hayakuwa na maji hali iliyofanya moto huo kuendelea kuteketeza soko hilo pamoja na mali zake. 

Yaraabh-Tobha, soko laisha wajameni.
Moshi mzito ulitanda.

No comments:

Post a Comment