Miaka ya siku nyingi kidogo wakati mimi (Caris) nikiwa bado mdogo kiasi, niliwahi kupita pembezoni mwa nyumba moja kubwa na kuu kuu hivi iliyokuwepo maeneo ya Tandika jijini Dar es salaam. Nyumba hiyo ilikuwa na baraza kubwa ya sakafu iliyotengenezwa vizuri tu ambapo vijana wengi (Jobless) walikuwa wakiitumia kama 'kijiwe' cha maongezi na mambo yao mengine (Pamoja na kwamba wenyeji walikuwa bado wanaishi ndani ya nyumba hiyo). Kutokana na uhuru waliokuwa nao vijana hao katika matumizi ya ile baraza, matokeo yake ni kuiacha baraza ile ikiwa chafu sana kila siku wanapoondoka hali iliyopelekea wenye nyumba kuweka tangazo lililokuwa limeandikwa kwa mkaa likisema "Ni marufuku kukaa na kula embe hapa" lakini cha kushangaza, baada ya siku chache akatokea mtu aliyejibu lile tangazo kwa kuhoji kwamba "Kwa nini tusile embe hapa?, na kwa kuwa swali lake lilikosa jibu, lile zoezi la kukaa na kula embe pale kwenye kibaraza likaendelea kudumu kwa muda mpaka ile nyumba ilipobomolewa.
Sababu ya mimi kuwashirikisha kwenye hadithi hii ya kisa cha kweli ni kulinganisha simulizi hiyo na kile kinachoonekana hapo pichani. Uzio huo ni wa soko jipya la Mwanjelwa linalojengwa ukiwa umewekewa kibao kinachosema "Marufuku kufanya biashara na kuegesha gari" ila mabegi ya wafanyabiashara ndio yamepata egemeo hapo...!!!??? What A Mess..?? Daaas Wots Up..!!
No comments:
Post a Comment