Tuesday, August 2, 2011

ZOMBE AAPA: CHADEMA IKISHIKA DOLA NITAJINYONGA MAKUSUDI:

Abdallah Zombe akizungumza na waandishi wa habari jana asubuhi.

Aliyekuwa kaimu kamishna wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la mahakama kuu jijini Dar es Salaam jana asubuhi, katika maelezo yake Zombe alisema kuwa anamshangaa mbunge wa Arusha mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya mambo ya ndani, ndugu Godless Lema, kwa kitendo chake cha kuhoji kuhusu uhalali wa hukumu ya Zombe katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge.
Zombe alisema kuwa, Lema hajui katiba ya Tanzania, akifafanua zaidi juu ya jambo hilo, alisema kuwa, Lema kama mbunge, bunge ni muhimili wa dola unaojitegemea na mahakama pia ni muhimili wa dola unaojitegemea, hivyo alishangaa kitendo cha Lema (MB) kuhoji maamuzi halali ya Mahakama.
Akiongeza alisema kuwa Wabunge wa CHADEMA hawajui watendalo bungeni na aliapa kuwa endapo Chadema watapata ridhaa ya kuongoza nchi, yeye Zombe atajinyonga kwa makusudi. "Endapo kama CHADEMA watatawala nchi hii, mimi nitajinyonga kabisa. Hiki ni chama cha hovyo na wabunge wake ni wa hovyo, hawaijui katiba hata kidogo", alisema Zombe.

No comments:

Post a Comment