Mwalimu wa shule ya msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro akisimamia mtihani jana asubuhi katika uwanja wa mpira wa miguu.
Katika hali isiyo ya kawaida,wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro jana asubuhi walinaswa na mtandao huu wakiwa wametapakaa kwenye uwanja wa mpira wakifanya mtihani huku wakiwa chini ya uangalizi mkali wa mwalimu wao.
Alipohojiwa na mwanidshi wa mtando huu juu ya wanafunzi hao kufanya mtihani kwenye uwanja huo, mwalimu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mazinda, alisema uongozi wa shule hiyo uliwapeleka wanafunzi hao kufanya mtihani huo uwanjani hapo kwa lengo la kuwapa nafasi ili wasiangaliane majibu.
''Tumeamua wafanye mtihani huu wa majaribio hapa kiwanjani kwa lengo la kuwapa uhuru zaidi kwani pale darasani huwa wanabanana, lakini sambamba na hilo, hali hii itasadia kwa wale wanafunzi wenye tabia ya kunakiri majibu kutoka kwa wenzao washindwe kufanya hivyo,'' alisema mwalimu huyo kwa kujiamini.
Hata hivyo, mwandishi wetu alishuhudia wanafunzi hao wakifanya mtihani huo kwa shida kubwa kwani walilazimika kuinama kwa muda wote wakiwa hapo.
Wengine wamebaki wakitafakari namna ya kuukabiiri mtihani huo katika mazingira hayo magumu.
Mtazamo wangu: Walimu kama hawa wanastahili kabisa kupewa adhabu ya viboko kama wale waliochapwa na mkuu wa wilaya fulani siku kadhaa zilizopita hapa nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment