Wednesday, July 6, 2011

MWANZA 'KIMENUKA', RISASI, MABOMU YA MACHOZI YAMEWAKA KUTAWANYA VURUGU ZA MACHINGA LEO HII, RAIA WENYE ASILI YA ASIA (HASA WAHINDI) TAABUNI :

Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.
Hapa Kushnei kabisaaa.

 Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
Friji baibai duniani.

 Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market na kisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.

 Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.
 Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza hali iliyopelekea kufungwa kwa soko hilo na biashara kusitishwa..


 Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.
 Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.
 Kamanda Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.
 Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.
 Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.
 Kuvunjwa vioo kwa jengo hili la msikiti wa hindu ni moja kati ya hasara zilizojitokeza.

Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment